Jumamosi 28 Februari 2026 - 00:40
Waislamu wa Uholanzi wanatumia fursa ya mwezi wa Ramadhani kuutambulisha Uislamu

Hawza/ Imeripotiwa kuwa wahubiri wa Kiislamu nchini Uholanzi wameanzisha mpango maalum katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kuitambulisha dini ya Uislamu na kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), kwa kuandaa mijadala ya wazi na wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Tukio hilo lilifanyika katika eneo la wazi la umma na lilijumuisha iftari ya pamoja, dua na maombi ya pamoja, pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja na wapita njia, kwa lengo la kujenga daraja kati ya jamii ya wenyeji na imani za Kiislamu.

Mpango huo uliandaliwa na chama kimoja cha kijamii cha eneo hilo, ambacho kilieleza kuwa hatua hiyo ilikuwa ni mwitikio wa tukio lililotokea katika mji wa Assen, ambapo nakala ya Qur’ani ilichomwa moto. Kitendo hicho kilizua hasira na huzuni kubwa miongoni mwa wananchi, na wengi walitoa wito wa kuimarishwa kwa mazungumzo badala ya makabiliano ya watu.

Wakati wa machweo, swala ya jamaa iliswaliwa kwa utukufu mkubwa, na baadaye Waislamu na wasio Waislamu walishiriki pamoja katika iftari na kushirikiana kijamii.

Washiriki walisisitiza kuwa; mazungumzo ndiyo njia bora ya kukabiliana na chuki na kuushinda mtazamo wa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), na kwamba kuwasilisha ukweli sahihi kunasaidia kuondoa mitazamo potofu na dhana zisizo sahihi kuhusu Uislamu.

Chanzo: International Union of Muslim Scholars

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha